Askofu Dr. Martin F. Shao

Askofu wa Tatu, Dayosisi ya Kaskazini

Mhe. Baba Askofu Dkt. Martin F. Shao amestaafu kwa heshima Februari 12, 2015 kwenye Usharika wa Lole wa K.K.K.T. Dayosisi ya Kaskazini jimbo la Kilimanjaro Mashariki, mara baada ya kulitumikia kanisa la Bwana kwa kipindi cha miaka 49. Askofu shao ametoa huduma kama mchungaji kwa miaka 12,  kama msaidizi wa Askofu kwa miaka 27 na kama Askofu kwa miaka 10.

Ibada iliongozwa na mkuu wa K.K.K.T. Dayosisi ya Kaskazini, Mhe. Baba Askofu  Dkt. Fredrick Shoo  na Tendo la Kumstaafisha Baba Askofu Martin Shao likafanywa na Askofu Dkt. Paul Akyoo akimwakilisha mkuu wa kanisa Dkt. Alex G. Malasusa.